Machapisho

UFAHAMU KUHUSU KISUKARI

Picha
“Elimika rejesha furaha yako’’ Na; Khalfan Ngeleja Kisukari ni ugonjwa unaotokana na ongezeko la sukari kwenye damu kuzidi kiwango cha kawaida ,kitaalamu hali hii huitwa (hyperglycemia) na husababishwa na vichochezi kedekede.kuna aina mbili za ugonjwa huu wa kisukari ambapo kuna aina ya kwanza inayofahamika kama (Diabetes mellitus type I), hii huhusiana na tatizo la homoni iitwayo insulini ambayo hutengenezwa na chembechembe za komgosho, kazi yake kubwa ni kuondoa kiasi kilichoongezeka cha sukari kwenye damu na kukiweka katika hali ya uhifadhi ili iweze kutumika kwa mahitaji ya mwili hapo baadae , kiasi cha sukari kitakachobadilishwa kitaalamu huitwa (Glycogen) . Wakati aina ya pili ya ugonjwa huu huitwa (diabetic mellitus type II) hutokea baada ya kuwepo kwa upingamizi wa kazi za homoni ya insulini na utengenezwaji wa homoni isiyo toshelevu kwa mahitaji ya mfumo wa mwili wako. Kuna ongezeko kubwa la uwepo wa ugonjwa wa kisukari duniani, inakadiliwa k